
Fundi wa TEHAMA
Hali: Alitoweka
Tarehe: 2020-01-01
Eneo: Shinyanga, Tanzania
Dennis alikuwa akifanya shughuli za TEHAMA kwa maana ya kutengeneza na kuuza computers, desktop pamoja na laptops na vifaa vingine vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ikiwemo CCTV.
Alifuatwa dukani kwake na watu wawili au zaidi waliolijitambulisha kuwa ni askari. Waliondoka kwa gari yake mwenyewe. Simu yake iliwashwa wilayani Musoma na baadaye gari yake ilikuja kupatikana wilaya ya Nzega baada ya wiki moja. Ni miaka 4 sasa imepita toka kutoweka kwake.
Ukumbusho wa Tanzania 2015 - 2025